Ni muhimu kwa mzazi/ mlezi kufahamu aina ya chakula kimfaacho mtoto wake hususani yule aliye katika umri wa miezi tisa na nusu mpaka miaka sita. Aina hizi za vyakula na jinsi ya uandaaji wake hutofautiana sana na zile anazokula mtoto mkubwa au mtu mzima. Leo, mtaalamu wetu wa mapishi, Chef Issa anatuletelea ratiba ya chakula cha mtoto wa umri huo.

Homa ya kweli inasababisha wasiwasi hasa katika miezi michache ya kwanza ya maisha ya mtoto. Hii ni kwa sababu mfumo wa kinga kwa watoto huwa bado mchanga na hauna ufanisi sana katika kupambana na maambukizi kwa miezi mitatu au minne ya mwanzo baada ya mtoto kuzaliwa.
Hivyo ni muhimu kujifunza namna sahihi ipasayo kuchukua joto la mtoto wako na kuelewa nini kinaashiria homa ya kweli.
Homa kwa mtoto
Kwa kawaida madaktari husema mtoto ana homa iwapo kama joto la mwili wake litaongezeka na kufikia nyuzijoto >37.5?? (99.5F) au zaidi. Ni vizuri kujua joto la kawaida la mtoto wako kwa kuchukua vipimo mara chache wakati mtoto yupo katika hali ya kawaida ‘mzima wa afya’.
Nini husababisha homa kwa watoto?
Kuna sababu kadhaa ziletazo homa kwa watoto. Upungufu wa maji mwilini ni mojawapo ya sababu hizo. Aidha joto la watoto wachanga linaweza kuwa juu kufuatia nguo nyingi alizovaa katika mazingira ya joto kiasi. Kwa kawaida inashauriwa mtoto wako avae safu moja zaidi ya mavazi zaidi ya yale ambayo wewe mwenyewe ukivaa yanakufanya ujisikie vizuri, maana yake ni kwamba kama wewe umevaa nguo mbili juu, na ukajisikia vema, basi mtoto wako avae walau nguo tatu ili kulinda joto lake lisipungue wala kuongezeka sana.
Sababu nyingine iwezayo kuleta homa kwa watoto ni maambukizi. Mfumo wa kinga ya mwili wa mtoto unapohisi kuingiliwa na vimelea vya maradhi kama vile bacteria au virusi, hutoa taarifa kwenye ubongo ambao nao hutoa kemikali fulani zinazosababisha joto kupanda mwilini. Kupanda kwa joto huko ambako huitwa homa kunaweza kuwa na faida kadhaa katika mwilini wa mtoto zikiwemo;
- Baadhi ya bakteria na virusi hawapendi hali ya joto la juu na hivyo basi ni rahisi zaidi kuharibiwa na mfumo wa kinga.
- Joto la juu la mwili husaidia mwili kupambana na maambukizi.
Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.
PID husababishwa na nini?
Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.
Je mwanamke huambukizwaje PID?
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na
- Kufanya ngono isiyo salama
- Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
- Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
- Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na
- Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
Dalili za PID ni zipi?
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni
Utangulizi
Ukweli ni kwamba karibu asilimia 3 ya watoto chini ya miaka 15 hupata degedege, nusu ya hawa hupata degedege linalosababishwa na homa kali. Kwa maana hiyo basi, degedege pia linaweza kumpata mtoto asiye na homa kama kifafa. Inakadiriwa kuwa mtoto 1 kati ya 100 hupata degedege la kifafa.
Degedege ni nini?
Degedege ni dalili inayoonesha mvurugano katika ufanyaji kazi wa seli za ubongo. Kwa kawaida, seli za ubongo ambazo kwa kitaalamu huitwa neurons huwasiliana kwa njia ya mtiririko wa umeme (electrical impulses). Ni mtiririko huu wa mawasiliano ya umeme kati ya seli za ubongo ndiyo unaofanya mwili uweze kufanya kazi ipasavyo. Iwapo basi itatokea kuwepo sababu yeyote ile itakayosababisha mawasiliano kati ya seli za ubongo kutokuwa katika mtiririko sahihi mfano kuwepo msisimko wa mawasiliano, hali hiyo husababisha degedege.
Degedege husababishwa na nini?
Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha degedege. Moja ya mambo yanayoweza kusababisha degedege ni kuwepo kwa jeraha katika ubongo (brain injury) ambalo linaweza kuwa kwa sababu yeyote ile ikiwemo jeraha analopata mtoto wakati wa kuzaliwa (brain ischemia).
Lakini pia kuna baadhi ya familia ambazo zinakuwa na matatizo ya kimaumbile katika ubongo zinazorithiwa toka kizazi hadi kizazi (mfano kifafa). Familia za namna hii huwa na watoto ambao hupatwa na degedege kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko familia ambazo hazina matatizo haya.
Vilevile degedege inaweza kuhusishwa na hali ya mabadiliko ya muda mfupi katika ubongo kama vile joto kali, matumizi ya madawa ya kulevya kama cocaine, amphetamine, viwango visivyo vya kawaida vya sukari na sodium katika damu (electrolytes imbalance) na uwepo wa uvimbe katika ubongo (brain tumor).
Sababu nyingine zinazoweza kusababisha degedege
- saratani ya ubongo,
- matatizo ya kimaumbile katika ubongo ya kuzaliwa nayo (congenital brain defects),
- mashambulizi ya vimelea vya bakteria, virusi, fangasi katika ubongo kama vile ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis).
Tunaendelea na mfululizo wa makala juu ya hali za dharura kipindi cha ujauzito. Leo tunazungumzia placenta previa.
Placenta previa ni miongoni mwa hali za hatari na dharura inayowapata baadhi ya mama wajawazito ambapo kondo la nyuma hujipachika katika sehemu ya chini ya mfuko wa uzazi, kukua na kisha kufunika sehemu ndogo au kubwa ya njia ya uzazi inayoelekea kwenye shingo ya uzazi na hivyo kuzuia kabisa uwezekano wa mtoto kuzaliwa kwa njia ya kawaida.
Chanzo chake ni nini?
Wakati wa ujauzito, kondo huongezeka ukubwa na kutanuka kadiri jinsi mfuko wa uzazi unavyotanuka na kukua. Kipindi cha awali cha ujazito, ni jambo la kawaida kwa kondo kuwa maeneo ya chini ya mfuko wa uzazi (low-lying palcenta). Lakini, kadiri mimba inavyokua ndivyo mfuko wa uzazi unavyopaswa pia kulivuta kondo kutoka sehemu za chini na kulipandisha sehemu za juu za kuta zake. Mpaka ifikapo theluthi ya tatu ya ujauzito, kondo linapaswa kuwa karibu kabisa na juu ya mfuko wa uzazi ili kufanya njia ya uzazi kuwa wazi kwa ajili ya kurahisisha utokaji wa mtoto.
Kucheua kwa mtoto ni hali ya mtoto kutoa chakula kupitia mdomoni muda mfupi baada ya kula/kunyonya.Kucheua kwa mtoto hupungua kadri mtoto anavyokuwa mkubwa na ni nadra sana kutokea baada ya mtoto kufikisha umri wa miezi 18.
Kucheua pia kunaweza kuashiria tatizo kubwa zaidi kwa mtoto kama ugonjwa wa Gastro-esophageal Reflux Disease (GERD), mzio (allergy) au kuziba kwa mrija wa kupitishia chakula.
Nini husababisha mtoto kucheua baada ya kula?
Masundosundo au vigwaru au Genital warts ni vinyama laini vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri. Vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo [urethra], vulva, shingo ya kizazi [cervix], au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.
Huu ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana [sexually transmitted infection (STI)].
Visababishi
Ugonjwa wa masundosundo husababishwa na jamii ya virusi wanaoitwa Human papilloma virus (HPV). Kuna zaidi ya aina 70 tofauti za virusi wa HPV ingawa si wote wanaosababisha masundosundo kwenye maeneo ya siri [genital warts]. Baadhi ya aina nyingine za HPV husababisha masundosundo kwenye ngozi inayozunguka sehemu nyngine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu.
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa baadhi ya aina za virusi wa HPV pia husababisha saratani ya shingo ya kizazi [carcinoma of the cervix] kwa wanawake au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer] kwa jinsia zote mbili. Aina hii ya virusi hujulikana pia kama high-risk HPV.
Pamoja na kwamba ugonjwa wa masundosundo kwenye maeneo ya siri umejitokeza kwa kasi kubwa hasa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI, watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile. Kwa mfano, kwa wanawake, virusi wa HPV wana uwezo wa kusambaa mpaka maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi [cervix] bila kuonekana wala kuhisiwa kwa urahisi.
Kama tulivyotangulia kueleza hapo awali, maambukizi ya HPV husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni. Mara baada ya kuambukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa masundosundo kuwa dhahiri, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yeyote ile. Aidha imeonekana pia kuwa si kila mtu anayejamiina na aliye na maambukizi ya HPV au mwenye masundosundo anaweza naye kupata ugonjwa huu.
Siku hizi, kumekuwa na taarifa nyingi juu ya masuala ya uzazi. Taarifa hizi hutokana na imani tofauti zilizopo kwenye jamii. Na, nyingi ya imani hizi hazina uhakika wa kitaalamu. Moja ya imani ni kutokukojoa kwa mwanamke baada ya tendo la ndoa ili kuzuia mbegu za kiume kutoka.
Kukojoa baada ya kufanya tendo la ndoa ni njia mojawapo inayotumiwa na wengi kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya njia ya mkojo (UTI). Na inashauriwa sana kukojoa punde baada ya tendo la ndoa ili kujikinga na uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa wa UTI kama anavyoelezea Dr. Leah Millheiser . Hivyo, kama na wewe ni mmoja wapo, basi unaweza kuendelea. Kukojoa baada ya tendo la ndoa hakuwezi kupunguza uwezekano wako wa kupata ujauzito.
Wakati wa tendo la ndoa, kuna mbegu kati ya milioni 20 hadi 400 hutotelwa na mwanamume kwenye manii (semen) kwa pamoja , na inakadiriwa kuwa mpaka 65% ya mbegu hufanikiwa kutoka kwenye bao na kuingia kwenye mlango wa uke ikisaidiwa na majimaji ya ukeni yanayotoka wakati wa tendo la ndoa (vaginal discharge) au kwa kitaalamu cervical mucus.
Asilimia kubwa ya mbegu hizi hupenya kwenye lango la uzazi wa mwanamke na kuacha sehemu kubwa ya manii ikiwa na maji maji mengine ambayo yana kiasi kidogo sana cha mbegu za kiume /shahawa (kumbuka manii za mwanamume zinajumuisha vitu vingi vingine zaidi ya shahawa kama protini , ute wa kusaidia shahawa kuelea au kwa kitaalamu Seminal fluid nk). Kwenye kila manii (bao) moja la mwanamume (manii yote unayoiona), inakadiriwa kuwa ni 1% tuu ndiyo shahawa / mbegu za mwanamume, hivyo unapoona kama manii zinamwagika, sehemu kubwa siyo mbegu bali ni majimaji mengine yanayotumika kwenye kuhifadhi mbegu za mwanamume.
Kumbuka: Shahawa(sperms) ni sehemu ya manii (semen ) inayotoka wakati mwanamume akifika kilele. Shahawa huelea kwa kutumia kimiminika kiitwacho Seminal fluid inayopatikana kwenye manii, Hivyo, siyo maji yote ya kwenye manii ni shahawa.
Kimsingi, mpaka muda anaenda kukojoa, mbegu huwa zimeshafika kwenye lango la uzazi, (cervix) hivyo kiasi kidogo sana cha mbegu zilizoshindwa kutoka kwenye manii ndiyo huendelea kubaki kwenye majimaji ambayo yatatoka dakika au masaa kadhaa baada ya tendo la ndoa.
Utangulizi
Kuharisha kwa watoto ni tatizo linaloshika nafasi ya pili duniani kwa kusababisha vifo miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano. Inakadiriwa kwamba kwa kila watoto 5 wanaofariki , 1 hufa kwa sababu ya kuharisha. Watoto milioni 1.5 kila mwaka hufa kutokana na kuharisha.
Leo hii, inakadiriwa asilimia 39 tu ya watoto wanaoharisha katika nchi zinazoendelea hupata matibabu sahihi.Hata hivyo, mwenendo wa kitakwimu unaonesha kwamba kumekuwa na mafanikio kidogo tangu mwaka 2000.
Kuharisha huelezwa kuwa ni upotevu wa maji na madini muhimu kwa mwili wa binadamu (electrolytes) kupitia kinyesi na kupelekea upungufu wa maji mwilini. Katika hali ya kawaida, watoto wachanga hutoa kiasi cha gramu 5 za kinyesi kwa kila kilo ya mtoto (5g/ kg) kwa siku, wakati mtu mzima hutoa wastani wa gramu 200 kwa siku.
Kati ya mambo ambayo watu wengi hawatilii maanani sana ni unywaji wa pombe wakati wa ujauzito. Nimekuwa nikiwaona akina mama wajawazito wengi wakinywa pombe kwenye sehemu za starehe na sherehe mbalimbali. Hata hivyo si nia ya makala hii kuwazuia kunywa pombe bali kuwapa elimu sahihi juu ya unywaji wa pombe wakati wa ujauzito.

