Dalili & Athari za Ugonjwa wa Virusi vya Corona
Dalili kuu za ugonjwa wa virusi vya Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu. Dalili kubwa na inayoweza kukufanya uhitaji uangalizi maalumu ni kukosa pumzi. Taarifa zinaonesha kuwa, ni mtu 1 kati ya watu 6 walioambukizwa virusi vya Corona hufikia dalili hii ya hatari. Na asilimia 80 ya walio na virusi hivyo hupata nafuu bila kuhitaji msaada wa matibabu.
Kifua kikavu & Mafua
Homa Kali
Kifua kubana / Upumuaji wa shida
Kukereketa kooni
Matatizo ya figo
Mwili Kuchoka sana
Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Virusi vya Corona
COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa binadamu. Kwa binadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji.
Vitu Unavyopaswa Kufanya
Osha mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni
Hakikisha unaosha mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni kwa muda usiopungua sekunde ishirini na ujikaushe kwa tishu utakayoitupa na wala si nguo yako. Kama hauwezi kupata maji basi tumia viua bakteria (sanitizers)
Vaa Barakoa (mask)
Tafiti zinaonyesha kuwa mask zina uwezowa kusaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona, hivyo inashauriwa utumie mask ili kuwalinda wengine haswa kwa wale wenye hofu ya kuwa na maambukizi.
Kinga pua na mdogo kwa tishu wakati wa kupiga chafya
Virusi vya Corona huweza kutoka na matone ya majimaji wakati unapopiga chafya, hivyo unashauriwa usipige chafya sehemu ya wazi au kwenye mikono, bali tumia tishu kavu kupigia chafya na uitupe sehemu husika baada ya hapo na unawe mikono kwa maji na sabuni au utumia sanitizers.
Vitu Usivyostahili Kuvifanya
Epuka safari na mikusanyiko isiyo ya lazima
Moja ya njia thabiti ya kuzuia maambukizi ya Corona ni kuepuka mikuanyiko isiyo ya lazima kama sherehe, harusi,makanisani, misikitini nk. Hii itasaidia kuzuia maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Epuka kupeana mikono au kujishika usoni
Pindi mtu mwenye virusi vya Corona atatoa matone (kwa kukohoa au kupiga chafya) Virusi vya Corona hukaa kwenye vitu (surface), hivyo kama utashika na ukajishika mdomoni, puani au machoni basi utajiambukiza virusi vya Corona. Kuepuka kushika uso ni moja ya njia thabiti ya kuepuka virusi hivi.
Epuka kusogeleana pindi uongeapo na mtu
Kwakuwa ni ngumu kumjua mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona. Hivyo inashauriwa kukaa umbali wa mita 2 pindi unapoongea na mtu. Hii itasaidia pindi akikohoa au kupiga chafya basi matone ya majimaji yanayobeba virusi hayawezi kukufikia kiurahisi.
Usambazaji wa Corona Virus
Pindi mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona akikohoa au kupiga chafya katika mkono wake na baadae kushika kitu kama kitasa cha mlango na wewe ukashika halafu ukajishika usoni kuna hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Corona. Wataalamu wanadhani kuwa virusi vya corona vinaweza kukaa kwa muda wa siku kadhaa. Hivyo tunashauriwa tunawe mara kwa mara na kuepuka kujishika usoni.
Kuwa Karibu na Mtu aliyeambukizwa
Pindi unapomuuguza au kuishi pamoja na mgonjwa wa Corona, una nafasi kubwa kupata ugonjwa huo. Hivyo, pindi unapojihisi kuwa umeambukiza,hakikisha unajitenga.
Matone ya chafya au Kikohozi
Virusi vya korona huweza kusafiri kupitia matone ya majimaji yanayotoka pindi unapokohoa au kupiga chafya, hivyo inashauri ukae umbali wa mita 2 pindi unapoongea na mtu.
Kushika sehemu zenye virusi
Kirusi cha Corona kina uwezo wa kukaa siku mbili juu ya kitu, hivyo pindi unapogusa kitu na kujishika usoni, unasafirisha virusi kutoka mikononi hadi mdomoni, puani au machoni.
Imani potofu kuhusu Corona
Pata uelewa sahihi juu ya corona na uepuke uzushi unaowafanya watu waishi kwa hofu au kuharibu njia za kujikinga
Ukipata Corona, kupona ni bahati
HAPANA, Idadi ya watu waliopona ni zaidi ya 80% huku idadi ya waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huu ikiwa chini ya 5%. Ugonjwa huu unaweza kumshambulia mtu yoyote, ila athari zake huwa kubwa zaidi kwa wazee au watu wenye matatizo ya kiafya.
Usipojitibu Corona ndani ya masaa 24 lazima utafariki
Nikinawa mikono kwa maji au viua bakteria (Sanitizer) siwezei kupata Corona
Corona haiwapati watu weusi
Joto huzuia Corona hivyo haiwezi kuenea katika nchi za joto
Ukipata Corona utashitakiwa na kuwekwa kifungoni
Corona huweza kutibiwa kwa maombi
Maswali ya mara kwa mara
Je umekuwa ukijiuliza ni njia gani au vitu gani muhimu kuhusu Corona bila majibu, pata ufafanuzi
Je ugonjwa wa Corona unatibika?
HAPANA, hadi sasa bado hakuna dawa iliyothibitika kutibu ugonjwa wa Corona..
Lakini, kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya viral infection, madaktari hutibu athari zinazoletwa na virusi vya Corona huku mwili ukiendelea kupambana navyo na hatimaye mgonjwa hupona na ugonjwa kuisha.
Lakini, kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya viral infection, madaktari hutibu athari zinazoletwa na virusi vya Corona huku mwili ukiendelea kupambana navyo na hatimaye mgonjwa hupona na ugonjwa kuisha.
Mask inasaidia kukinga na Corona
Je ninaweza kuambukizwa Corona kwa kupokea barua au mzigo kutoka ng'ambo?
Kuna utofauti gani kati ya corona na mafua?
Corona inaambukiza zaidi ya mafua?
Ninaweza kupata corona kupitia chakula
Nichukue tahadhari gani?