Image

Tatizo la kufunguka mlango wa kushoto wa moyo unaotenganisha chumba kidogo na kikubwa cha moyo na  kuzuia  kupita kwa damu ya kutosha kwenda kwenye mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ambao huhusika kuzungusha damu ndani ya mwili hujulikana kama mitral stenosis

Visababishi

Tatizo hili la kufunguka mlango wa kushoto wa moyo unaotenganisha chumba kidogo na kikubwa husababishwa na;

  • Homa inayojulikana kama rheumatic fever
  • Mtu anaweza kuzaliwa na hali hii
  • Matibabu ya saratani za kifua kwa kutumia tiba ya mionzi
  • Mkusanyiko wa madini aina  calcium kwenye milango hiyo ya moyo

Kati ya hizi sababu hapo juu, inayosababisha kutokea kwa  tatizo hili kwa wakubwa ni homa ya rheumatic fever, ambayo hufuatia maambukizi ya vimelea vya bakteria aina ya  streptococci kwenye koo au ngozi ambayo hayakutibiwa kikamilifu

 

 Shinikizo la damu ni moja ya tatizo linaloathiri watu wengi duniani.

Nini maana ya shinikizo la damu?

Ni msukumo wa damu ulioko juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huitajika mwilini ili kusambaza chakula,oksijeni na kutoa uchafu.

Uanishaji wa shinikizo la damu

Uanishaji

Systolic BP

Diastolic BP

Kawaida (normal)

<120

<80

Prehypertension

120-139

80-89

Kali (mild hypertension)

140-159

90-99

Kali kiasi (moderate hypertension)

160-179

100-109

Kali sana (severe Hypertension)

≥180

≥110

Shinikizo la damu hupimwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer

Shinikizo la damu husababishwa na nini?

Aina ya kwanza

Asilimia 90-95 sababu huwa hazijulikani na kitaalamu huitwa primary or essential hypertension. Ingawa vitu vifuatavyo vimehusishwa kupelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu. Navyo ni:

  • Uvutaji sigara
  • Unene (visceral obesity)
  • Unywaji wa pombe
  • Upungufu wa madini ya potassium
  • Upungufu wa vitamin D
  • Kurithi
  • Umri mkubwa
  • Chumvi na madini ya sodium kwa ujumla
  • Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
  • Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

Aina ya Pili

Asilimia 5 huwa na sababu dhahiri zinazopelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu na huitwa kitaalamu secondary hypertension. Na sababu hizi ni:

  • Hali ya kukosa hewa usingizini (sleep Apnea)
  • Kasoro ya kuzaliwa nayo katika mshipa mkubwa wa damu (Coarctation of Aorta)
  • Saratani za figo (wilm’s tumor, renal cell carcinoma)
  • Saratani ya tezi iliyo juu ya figo (pheochromocytoma)
  • Ujauzito – wapo wakina mama wajawazito ambao hupata shinikizo la damu na huwa hatarini kupata kifafa cha mimba (eclampsia)
  • Magonjwa ya figo (renal artery stenosis, glomerulonephritis)

Dalili

Mara nyingi huwa hamna dalili zozote, na kama zikiwepo mgonjwa huwa na dalili zifuatazo

  • Uchovu
  • Maumivu ya kichwa
  • Kuhisi mapigo ya moyo kwenda haraka
  • Kichefuchefu
  • Kutapika
  • Damu kutoka puani
  • Kutoweza kuona vizuri (blurred vision)
  • Kusikia kelele masikioni
  • Na mara chache kuchanganyikiwa

Vipimo na uchunguzi

Huitaji kupima angalau mara tatu angalu wiki moja tofauti ilikuweza kusema mgonjwa ana shinikizo la damu kwa kutumia kifaa kinachoitwa kitaalamu Sphygmomanometer. Vipimo vingine ni:

  • Damu kuchunguza wingi wa lijamu mwilini (cholesterol), na pia vitu kama (BUN, na electrolytes)
  • Kipimo cha mkojo (Urinalysis)
  • Electrocardiogram (ECG)
  • Echocardiography
  • Ultrasound ya mafigo

Matibabu

Lengo ni kuzuia madhara ambayo yanaweza kuletwa na shinikizo la damu. Dawa zifuatazo hutumika kutibu shinikizo la damu: dawa jamii ya Alpha blockers, dawa jamii ya Angiotensin converting enzyme inhibitor (ACEI), dawa jamii ya Angiotensin receptor blocker (ARB), dawa jamii ya Beta blocker, dawa jamii ya Calcium channel blocker, dawa jamii ya Diuretics, dawa jamii ya Renin inhibitors na dawa jamii ya Vasodilators.

Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu

  • Kiharusi
  • Moyo kushindwa kufanya kazi ( congestive heart failure)
  • Madhara katika mshipa mkubwa wa damu ambapo ukuta wa ndani huchanika na damu hukusanyika katika ukuta wa mshipa huo(aortic dissection)
  • Magonjwa ya mishipa ya damu
  • Kushindwa kuona
  • Athari katika ubongo

Jinsi ya kuzuia shinikizo la damu

Chakula cha afya kisicho na mafuta mengi na chenye madini ya potassium kitaalamu kinaitwa DASH diet (dietary approaches to stop hypertension)

  • Mazoezi mara kwa mara- angalau nusu saa kwa siku
  • Kwa wavutaji sigara kuacha kuvuta sigara
  • Punguza au kama unaweza acha unywaji wa pombe ( kwa wanaume angalau bia 2 kwa siku na wanawake bia 1)
  • Punguza utumiaji wa chumvi hasa ya kuongeza mezani (usitumie zaidi ya gramu 1.5)
  • Punguza msongo mawazo
  • Hakikisha unakuwa kwenye uzito wa afya, kama uko kwenye uzito wa hatari fanya mpango wa kupunguza uzito.
  • Matumizi ya mafuta ya samaki husaidia kupunguza shinikizo la damu, kwa wenye shinikizo la damu.

Moja ya magonjwa hatari sana ambayo yanaweza kumpata mtu yoyote ni ugonjwa wa shambulizi la moyo. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanaume na wanawake.

Kwa kawaida, ugonjwa huu hutokea pale ambapo sehemu ya nyama ya moyo inapoharibika au kufa kutokana na kukosa damu ya kutosha.

Je tatizo hili husababishwa na nini?

Husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo (coronary artery blockage) kutokana na mafuta mabaya mwilini (atherosclerotic plaque).

Watu gani wapo katika hatari ya tatizo hili?

Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na

  • Wenye umri mkubwa miaka 45 kwa wanaume na 55 kwa wanawake
  • Wavutaji wa sigara
  • Watu wenye mafuta ya lijamu katika damu au wale wenye mafuta mabaya aina ya triglycerides na low density lipoprotein kwa kiwango kikubwa katika damu zao
  • Wenye kisukari
  • Wenye matatizo ya shinikizo la damu
  • Walio na unene kupita kiasi (obesity)
  • Wenye matatizo sugu ya kushindwa kufanya kazi kwa figo zao (chronic renal failure)
  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
  • Wanywaji wa pombe kupindukia
  • Watumiaji wa madawa ya kulevya hasa cocaine na methamphetamine
  • Watu wenye msongo wa mawazo (Chronic high stress levels)
  • Upungufu wa vitamin B2, B6, B12 na folic acid

Dalili za shambulizi la moyo

  • Maumivu makali ya ghafla kifuani ambayo husambaa kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto
  • Kupumua kwa shida
  • Kutoka jasho kwa wingi sana (diaphoresis)
  • Kuhisi mapigo ya moyo yanapiga haraka (palpitations)
  • Kichefuchefu
  • Kutapika
  • Kuchoka haraka sana
  • Kupoteza fahamu

Shambulizi la moyo limehusishwa na nini?

Tafiti mbalimbali zimeusisha mambo yafuatayo na shambulizi la moyo

  • Msongo wa mawazo
  • Maambukizi hasa vichomi vinavyosababishwa na vimelea vya chlamydophila pneumonia.
  • Hutokea zaidi asubuhi hasa saa tatu (saa 3 asubuhi)

Vipimo na uchunguzi

  • ECG - Kipimo hiki huonyesha ni sehemu gani ya moyo iliyoathirika
  • Coronary angiography - Kinasaidia kwa kuangalia wapi ambapo mishipa ya damu imekuwa membamba sana kupita kiasi (narrowing of vessels) au imeziba.
  • Cardiac markers levels
  • X-ray ya kifua (chest X-ray)
  • MPI (Myocardial Perfusion Imaging) - Kipimo hiki hufanywa kwa kutumia mashine maalum ya PET Scan ambapo kinauwezo wa kugundua tatizo la shambulizi la moyo, huchunguza kikamilifu maumivu ya kifua, huangalia mwelekeo wa tiba ya kuzuia damu kuganda, hutoa mwelekeo wa ugonjwa wa shambulizi la moyo kama ni mzuri au mbaya, hutathmini ubora wa tiba ya shambulizi la moyo kabla na baada ya mgonjwa kupata tiba, huweza kutambua hata shambulizi la moyo ambalo si rahisi kugundulika kwa kutumia vipimo vyengine na pia hutathmini ukubwa wa tatizo la shambulizi la moyo. Hata hivyo kwa sasa kipimo hiki hakipatikani nchini kwetu.

Ili kuweza kutambua uwepo wa tatizo hili, mwaka 1979, shirika la Afya Duniani (WHO) liliweka vigezo vya kutambua shambulizi la moyo.

Vigezo hivyo ni

  • Historia ya kuwa na maumivu ya kifua zaidi ya dakika 20
  • Mabadiliko katika kipimo cha ECG, na
  • Kupanda na kushuka kwa kipimo kiitwacho kitaalamu cardiac biomarkers hasa creatine kinase - MB na troponin

Matibabu

Shambulio la moyo ni tatizo linalohitaji matibabu ya dharua. Lisipotibiwa kwa haraka husababisha kifo katika muda mfupi sana tangu mgonjwa apatwe na tatizo. Matibabu ya tatizo hili hujumuisha

  • Kumpa mgonjwa hewa ya oksijeni
  • Mgonjwa hupewa vidonge vya Aspirini ndogo kuzuia damu kuganda (thrombolytic) kwa ajili ya kuyeyusha damu iliyaganda na hivyo kuzibua mirija midogo ya damu katika moyo iliyozibwa na kuganda huku kwa damu.
  • Vile vile mgonjwa hupewa dawa za kuweka chini ya ulimi kiitwacho nitrogylycerin (glyceryl trinitrate) ambazo husaidia kutanua mishipa ya damu (vasodilation)
  • Dawa ya kutuliza maumivu kwa mfano morphine
  • Dawa ya kuyeyusha mafuta katika mishipa ya damu kama vile clopidogrel
  • Kuzibua mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo kwa kutumia - Percutaneous coronary intervention (PCI)
  • Upasuaji (CABG)

Njia za kuzuia shambulizi la moyo

  • Kuacha kuvuta sigara
  • Kufanya mazoezi ya mara kwa mara
  • Kupunguza unywaji wa pombe
  • Kubadilisha aina ya mlo. Kupunguza mafuta katika mlo na chumvi.
  • Kutumia mafuta ya samaki (omega-3 fatty acids)
  • Kuna utafiti unaosema kuwa uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.

Madhara ya shambulizi la moyo

  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
  • Matatizo katika mfumo wa mapigo ya moyo (Atrial fibrillation) ambayo hatimaye hupelekea kifo
  • Shambulizi la moyo kurudia mara ya pili
  • Kifo cha ghafla (sudden death)

Daktari mmoja aitwaye Mackod, alipitia makala nyingi za afya ili kuweza  kutambua visababishi vya vifo ambayo havitokani na umri au nasaba ya kiasili (Genetic), na akagundua mambo tisa ambayo yanasabisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika. Mambo hayo tisa ni; uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, kutofanya wa mazoezi, lishe duni, wadudu kama bakteria na virusi, ajali, tabia za ngono za kupita kiasi bila kinga,  vita na madawa ya kulevya.

Katika makala hii ningependa kuzungumzia juu ya ufanyaji wa wazoezi na hasa wakati bora wa kufanya mazoezi. Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kupunguza mafuta ya ziada mwilini, tafiti zinaonesha kuwa asiyefanya mazoezi, madhara anayopata ni sawa na mtu anayevuta tumbaku.

Utafiti uliofanywa na Dr. Jason na Nor Farah (2004) wa Chuo kikuu cha Glasgow, umeonesha kuwa unapofanya mazoezi kabla ya kifungua kinywa, wakati tumbo likiwa tupu, ni bora zaidi kuliko unapoweza kufanya mazoezi baada ya mlo wowote. Kufanya mazoezi ni jambo la maana kwa afya kuliko kutokufanya mazoezi ya mwili, lakini unaweza kupata  faida zaidi kama unaweza kufanya kabla hujala chochote.

Mazoezi kwa ujumla wake yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yakiambatana na lishe bora. Mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, kansa na shinikizo la damu, pia kwa kufanya mazoezi unaweza kuongeza kipato kwa kuwa unaweza kufanya kazi muda mrefu kuliko asiyefanya mazoezi.

Familia ambazo hufanya mazoezi huwa na afya bora na kipato kikubwa kwa kuwa fedha kidogo wanazopata hutumika kwenye maendeleo tofauti na familia zisizofanya mazoezi ambazo hujikuta wakitumia kipato hicho kidogo kwa ajili ya kutibu  magonjwa ambayo yangeepukika kwa kufanya mazoezi.

Katika tafiti mpya zilizofanywa hivi karibuni zinaonyesha kuwa unyongovu na jaribio la kujiua ni viashiria hatari ambavyo huleteleza vijana kufa kwa magonjwa ya moyo.

Katika utafiti mkubwa uliohusisha washiriki zaidi ya 7000 walio chini ya miaka 40 ulionyesha kuwa kwa wale waliokuwa na historia ya unyongovu au jaribio la kujiua walikuwa na hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na magonjwa ya moyo hasa yale ambayo moyo hukosa oksijeni ya kutosha (ischemic heart disease) ukilinganisha na wale ambao hawakuwa na historia hiyo.

Ingawa jinsia zote zilikuwa kwenye hatari zaidi ya kufa kutokana na magonjwa ya moyo, lakini wanawake wenye unyongovu au waliofanya jaribio la kujiua walikuwa na hatari mara 14 zaidi ya kufa kwa magonjwa ya moyo yatokanayo na kukosa oksijeni ya kutosha (ischemic heart disease) kulinganisha na wale ambao hawakuwa na unyongovu au jaribio la kujiua.

Katika utafiti huu uliofanywa na Profesa Viola Vaccarino kutoka chuo kikuu cha Emory, Atlanta, Georgia aligundua jinsi matatizo ya kisaikolojia yanavyopelekea kuongeza hatari ya kufa mapema na magonjwa ya moyo katika idadi ya vijana.

Taarifa nyingi zilizopo za magonjwa ya moyo ambazo zilizokwisha tolewa huwa za umri wa kati na wazee, maana imekuwa ikizoeleka magonjwa haya huathiri zaidi rika hiyo, ambayo ni kweli kabisa hasa katika magonjwa yanao athiri zaidi mishipa ya damu ya moyo (CHD).

Makala ya leo ni muendelezo wa magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, na ugonjwa wa leo hujulikana kama Tundu katika moyo, au Tundu katika kuta za ventrikali za moyo, ni ugonjwa ambao hutokea mara nyingi zaidi.

Watoto wenye tundu dogo katika moyo, huweza kukua bila matatizo yoyote, wakati wale wenye tundu kubwa huanza kuonesha dalili mapema

Vifuatavyo ni vihatarishi ambavyo vinaweza kupelekea kupata tundu katika kuta za chini za moyo

  • Maambukizi ya Rubella katika kipindi cha ujauzito
  • Ugonjwa wa kisukari ambao haujadhibitiwa kwa mama mjamzito
  • Matumizi ya pombe au madawa ya kulevya na baadhi ya dawa za hospitali katika kipindi cha ujauzito

Dalili

  • Rangi ya ngozi, midomo na kucha hubadilika na kuwa bluu
  • Kunyonya au kula kwa shida sana, na ukuaji wa shida
  • Kupumua kwa shida
  • Kuchoka haraka
  • Kujaa miguu na kuvimba tumbo
  • Mapigo ya moyo ya haraka
  • Kwa mtaalamu anaweza kusikia ishara ya ongezeko la sauti ya ziada ya mapigo ya moyo ya mtoto hali ambayo wataalamu huiita holosystolic murmur kwa kutumia kifaa kitaalamu stethoscope

Madawa ya kulevya yameleta athari sana katika jamii, kutokana na ile hali ya kufanya hisia ya utegemezi, kwamba mtu anaona hawezi kufanya chochote bila kupata japo kidogo.

Kuna aina nyingi za madawa ya kulevya ila aina mbili ndio ambayo yanasumbua sana,

  • Cocaine
  • Heroin

Cocaine hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamu Erythroxylon coca, na huandaliwa kwa kupitia hatua mbali mbali na hatua moja wapo ni ya kupata kinachotumika kuengenezea soda za cola, na hatua ya mbele zaidi ndio cocaine. matumizi yake ni kwa kujichoma sindano, na wengine huvuta aidha kwa kuunguza kwanza ambao huitwa‘crack’ , mpaka mwaka 2007,Marekani ilikuwa na watumiaji million 2.1, na kati ya hao million 1.6 walikuwa tegemezi au mateja , na matumizi ya kawaida au ya kupitiliza ya cocaine yalipekea asilimia 30% kuhudhuria hospitali kutokana na athari zake, na wengi hufika hospitali wakilalamika maamumivu makali ya kifua.

Kutoka katika jarida la Circulation Vol.122, issue24 liliotolewa Desemba 2010, waliripoti kati ya wagonjwa 233 ambao ni watumiaji wa cocaine katika idara ya dharura asilimia 56% walikuwa na athari kwenye moyo na asilimia 40% walilalamika kuwa na maumivu ya kifua. Taarifa za hvivi karibuni inaonyesha marekani ina watu milion 30 ambayo wametumia cocaine na milioni 5-6 ni tegemezi au mateja (taarifa kutoka jarida la national medical association)

Heroin hutoka kwenye ua kitaalamu hujulikana papaver somniferum- opium poppy, katika karne ya 18, madaktari walitumia kama dawa ya kupunguza maumivu hasa kwa wagonjwa wa saratani, pepopunda, hedhi. Mwishoni mwa karne ya 18 ndio madaktari waligundua hali ya tegemezi ya kulevya iliyoletwa na heroin.  Huandaliwa kupitia hatua mbali mbali na hatua moja wapo ni dawa ambayo hutumiwa kupunguza maumivu kitaalamu Morphine, na hatua za mbele zaidi ndio heroin.  Heroin hutumika kwa njia ya kunusa na kuvuta puani na kujichoma sindano

Cocaine na Heroin zote hulevya kukupa hali ya kujisikia furaha kitaalamu Euphoria, ila hupelekea kuwa tegemezi wa kulevya huko.

Hutokea pale vimelea (bakteria) wanapovamia kuta za ndani za moyo (endocardium), zikiwepo valve na kusababisha maambukizi.

Hakuna mishipa ya damu ambayo ni mahususi kwa ajili ya kupeleka damu safi moja kwa moja kwenye valve za moyo, hivyo chembe chembe nyeupe za damu (ambazo ni mahususi kwa ajili ya kinga ya maambukizi) hufika kwa shida sana kwenye valve za moyo. Hali hii husababisha chembe chembe nyeupe kuwa butu  pale vimelea (bakteria) wanapotengeneza uoto (vegetations) kwenye valve za moyo. Na kwa sababu ya hakuna mishipa ya damu ambayo ni mahususi kwa ajili ya kupeleka damu moja kwa moja kwenye valve za moyo, matibabu yake husumbua sana kwakuwa ni vigumu dawa kufika kwenye eneo husika.

Maambukizi katika kuta za ndani za moyo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili kutokana na  jinsi ugonjwa ulivyo-anza (onset):

Maambukizi ya kuta za ndani za moyo ya papo kwa hapo kitaalamu acute bacteria endocarditis 

huanza kati ya siku kadhaa hadi wiki kadhaa, na mgonjwa huwa maututi; na maambukizi katika kuta za ndani za moyo ndogo ya papo kwa hapo kitaalamu sub acute bacteria endocarditis- huanza kati ya wiki kadhaa hadi miezi kadhaa, na dalili hutokea pole pole

Na vile vile maambukizi haya yanaweza kugawanywa kama ifuatavyo

  • Maambukizi katika kuta za ndani za moyo ya Valve asili au kitaalamu native valve endocarditis
  • Maambukizi katika kuta za ndani za moyo ya Valve za bandia au kitaalamu prosthetic valve endocarditis
  • Maambukizi katika kuta za ndani za moyo kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya kwa njia ya mshipa kitaalamu intravenous drug abuse endocarditis

Raia mmoja nchini Italia mwenye umri wa miaka 71 alipata mishtuko ya mioyo yake yote miwili na kupoteza fahamu kwa sekunde kadhaa lakini hatimaye aliweza kuokolewa maisha yake. Mtu huyo alikimbizwa katika hospitali ya Verona nchini Italia baada ya kupata maumivu ya kifua na mapigo ya mioyo yake kuwa si ya kawaida.

Taarifa kutoka jarida la American Emergency Medical Journal inaeleza kuwa mtu huyo aliwahi kufanyiwa upasuaji wa moyo na kupandikizwa moyo mwingine miaka kadhaa iliyopita katika upasuaji unaojulikana kama double heart transplant (heterotopic heart transplantation).

Hii ni aina ya upasuaji ambapo moyo hupandikizwa na kufanya kazi sambamba na moyo wa awali (wa mgonjwa mwenyewe) ambao huwa umeadhirika kutokana na maradhi. Chemba za damu za kwenye mioyo hiyo huunganishwa ili moyo uliopandikizwa uweze kusaidia moyo wa mgonjwa.

Ripoti zinasema kuwa moyo mmoja ulianza kuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine na hivyo kusababisha mapigo yake kutofautiana na mwingine. Madaktari walijaribu kurekebisha mapigo ya mioyo hiyo ili yaendane sawa kwa kutumia dawa lakini mioyo hiyo iliacha kupiga kabisa na mtu huyo kuacha kupumua.

Hata hivyo, waliweza kumrejesha katika hali ya kupumua kwa kutumia kifaa maalum cha Defibrillator kabla ya kumfanyia upasuaji na kubadilisha kifaa kinachosaidia kuweka sawa mapigo ya moyo kinachojulikana kama pacemaker.

Katika muendelezo wa magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, leo nitagusia kuhusu Tundu katika kuta za juu za moyo (atrial walls) au kwa kitaalamu Atrial septal defect (ASD).

Wakati kijusi (fetus) kinapo endelea kukua, kuta kati ya atria mbili za moyo nayo hukua (kitaalamu interatrial septum) ili kutenganisha chemba ya kulia na kushoto. Lakini katika kipindi hiki huwa kuna tundu kati ya kuta hizi kitaalamu huitwa foramen ovale.

Tundu hili ni la kawaida kwa kipindi hiki cha kijusi, tundu hili husababisha damu yenye oksijeni  kutoka kwenye kondo la mama (placenta) kutokwenda kwenye mapafu amabayo hayaja komaa na kuelekea sehemu nyingine za mwili hasa kichwani. Kipande cha tishu kinachoitwa kitaalamu septum primum hufanya kazi kama valvu katika tundu hili. Mara tu mtoto anapozaliwa, shinikizo katika mishipa ya damu ya mapafu (pulmonary circulatory system) hushuka na kusababisha tundu hili (foramen ovale) kufunga kabisa.

Tundu hili huwa halifungi kabisa kwenye karibu asilimia ishirini na tano ya watu wazima, hivyo pindi shinikizo likiongezeka katika mishipa ya damu ya mapafu (hali inayoweza kutokea kwa sababu ya kuwepo kwa shinikizo la damu kwenye mapafu (pulmonary hypertension) kutokana na sababu mbalimbali, au kuwa na matatizo ya kikohozi cha muda mrefu), husababisha tundu la foramen ovale kutofunga na kubaki wazi. Hali hii kitaalamu huitwa patent foramen ovale (PFO).

Aina za tundu katika kuta za juu za moyo

Mpaka sasa, zipo aina kuu sita za tundu katika kuta za juu za moyo, ambazo ni

Ukurasa 1 ya 2