Image

Kutokupata choo au kuhisi kwenda kujisaidia haja kubwa na kutofanikiwa kutoa choo au mtu kupata choo chini ya mara tatu kwa wiki hujulikana kitaalamu kama constipation.Mtu mwenye tatizo hili la kufunga choo hupata choo kigumu,kikavu na chenye kupita kwa taabu kwenye njia ya haja kubwa

Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba angalau kila mtu katika maisha yake huwa anapata tatizo hili la kufunga choo. Kufunga choo ni tatizo ambalo watu wengi  bado huhisi ni jambo la aibu sana hata kulizungumzia na hubaki na tatizo kwa muda mrefu  mpaka pale wanapopata madhara ya kiafya ndio hutafuta msaada wa kitabibu.

Dalili  zifuatazo zinaweza kutumika kuelezea tatizo la choo kufunga;

  1. Kupata choo kigumu na kinachoambatana na maumivu makali wakati wa kwenda haja kubwa
  2. Kutokupata choo kwa muda mrefu (infrequent bowel movements)
  3. Mtu kuhisi kama hajamaliza haja kubwa licha ya kupata choo

Tafiti nyingi zilizowahi kufayika zinaonyesha kwamba takribani asilimia 16 (16%) ya watu wazima hupata tatizo hili la kufunga choo,waathirika wengi wakiwa ni watu wenye umri kati  ya 60-110 (asilimia 35%).

Kwa nini wazee hupata tatizo hili la kufunga choo?

Sababu zifuatazo huchangia wazee kutokupata choo au kufunga choo;

  1. Hali ya uzee husababisha mmeng’enyo wa chakula kufanyika taratibu (slow metabolism) 
  2. Ukosefu wa lishe bora
  3. Kutokunywa maji ya kutosha
  4. Kutofanya mazoezi
  5. Magonjwa ya uzee kama pelvic floor prolapse na utumiaji wa dawa aina ya antacids na dawa za kupunguza maumivu
  6. Pia uzee husababisha meno kung’oka hivyo wazee huchagua vyakula laini na vyenye ufumwele (fiber) kidogo

Wanawake wajawazito ni miongoni mwa watu wanaopata tatizo hili la kufunga choo mara kwa mara.

Visababishi vya choo kufunga (constipation) ni kama ifuatavyo;

  1. Kutokula mlo wenye ufumwele (fiber) wa kutosha
  2. Kutokunywa maji ya kutosha
  3. Kutumia sana dawa za kulainisha choo
  4. Kutokufanya mazoezi au
  5. kuishi maisha ya unyongovu (stressful life)
  6. Madawa kama aspirin (NSAID), morphine, dawa za presha(thiazides, verapamil, furosemide), dawa za sonono (antidpressants), madawa ya saratani n.k
  7. Magonjwa ya  mfumo wa mmengenyo wa chakula  au  vichocheo vya mwili (hormonal disorders) kama hypothyroidism
  8. Ujauzito- Mama mjamzito yupo kwenye hatari zaidi ya kupata choo kigumu au constipation hasa katika miezi ya mwisho ya ujauzaito wake kwa sababu ya kuongezeka kwa vichocheo mwili aina ya sex hormones, kupungua kwa mmeng’enyo kwenye tumbo na kuchelewa kwa tumbo kupitisha chakula (delayed interstinal emptying)
  9. Magonjwa ya tumbo kama colorectal dysfunction, diverticulitis, irritable bowel syndrome, saratani za matumbo hasa utumbo mkubwa
  10. Chronic Idiopathic constipation- Sababu zisizojulikana

Kama ambavyo tumejifunza sababu na makundi wa watu ambao wapo kwenye hatari zaidi. Tatizo hili linaweza kumpata mtu yoyote wa rika lolote hata watoto wachanga. Hivyo fuatilia makala zetu zijazo ili kujua uchunguzi,matibabu na jinsi ya kuepukana na tatizo hili la kufunga choo.Kama tayari una tatizo hili  tafadhali fika kituo cha afya kilichokaribu nawe kwa ajili ya uchunguzi, matibabu na ushauri wa kitaalamu.

Baadhi ya watu hukumbwa na tatizo la kuwa na vijiwe katika figo na mfumo wa mkojo kwa ujumla. Mawe haya hutokana na ama madini chumvi au tindikali mbalimbali zinazotolewa mwilini.

Aina za mawe katika figo

Aina za vijiwe katika figo ni pamoja na

  • vijiwe vya calcium oxalate
  • vijiwe vya tindikali ya uric (uric acid)
  • Vijiwe vya struvite (magnesium, ammonium na phosphate)

Vijiwe katika figo husababishwa na nini?

Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini yaani electrolyte imbalance.

Kuharibika kwa chujio ama Glomerulonephritis ni aina ya ugonjwa wa figo unaoathiri sehemu maalum ya figo (chujio) inayohusika na uchujaji wa maji pamoja na uchafu kutoka katika damu. Sehemu hii huitwa glomelurus au chujio kama tutakavyokuwa tukitumia katika mada hii. 

Visababishi

Mara nyingi chanzo halisi cha kuharibika kwa chujio za figo (glomerulonephritis) huwa hakijulikani. Hata hivyo wakati mwingine uharibifu huu unaweza kusababishwa na kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili. Uharibifu katika chujio husababisha damu pamoja na protini kuingia katika mkojo. 

Tatizo hili hukua kwa haraka na figo linaweza kupoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kwa kasi ndani ya muda mfupi wa kati wiki chache mpaka miezi kadhaa. Aina hii ya kuharibika kwa chujio za figo kwa haraka hujulikana kitalaamu kama rapidly progressive glomerulonephritis. 

.

Ukubwa wa tatizo na vihatarishi vyake

Takribani robo ya watu wanaopatwa na tatizo sugu la glomerulonephritis huwa hawana historia ya kuwa na ugonjwa wowote wa  figo hapo kabla. 

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kumfanya mtu awe katika hatari ya kupata glomerulonephritis. Mambo hayo ni pamoja na:

  • Matatizo katika mfumo wake wa damu au lymph
  • Kuwahi kutumia vimiminika vilivyotengenezwa kwa kemikali za hydrocarbon
  • Wenye historia ya saratani
  • Maambukizi ya bakteria aina ya streptococcus, virusi, majipu au maambukizi katika moyo 
  • Mambo mengine yanayoweza kuongeza hatari ya kupatwa na glomerulonephritis ni pamoja na:
  • Magonjwa ya mishipa ya damu kama vile vasculitis au polyarteritis
  • Matumizi yaliyopitiliza ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non steroidal anti-inflammatory drugs kama vile aspirin na diclofenac
  • Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili kama vile Anti-glomerular basement membrane antibody disease na IgA nephropathy
  • Makovu katika chujio (Focal segmental glomerulosclerosis) au hali ya chujio kuwa na kuta nene kuliko kawaida (Membranoproliferative GN)
  • Magonjwa yanayoathiri viungo mbalimbali vya mwili kama vile Henoch-Schonlein purpura, IgA nephropathy, Goodpasture’s syndrome au Lupus nephritis 
  • Ugonjwa wa kimetaboliki wa Amyloidosis

 Dalili

Dalili kuu za glomerulonephritis ni kuwa na damu katika mkojo (hali inayoufanya mkojo kuwa na rangi kama nyeusi, kutu au samawati; mkojo kuwa kama wenye povu jingi (kwa sababu ya kuwa na protini nyingi kuliko kawaida) na kuvimba uso, macho, miguu au tumbo (hali inayojulikana kama edema) 

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu.

Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo. Aidha tafiti zinaonyosha takribani asilimia 70 za madoda ya tumbo hazionyeshi dalili yoyote. mara nyingi aina hii ya tukia (presentation) hupelekea madhara makubwa kwa ghufla kama madonda kutoa damu (bleeding) na matumbo kutoboka (perforation)

Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kama Helicobacter pylori. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-inflamatory Drugs kama aspirin au diclofenac huweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoathiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum.

Neno syndrome humaanisha mkusanyiko wa dalili au magonjwa kadhaa ili kufanya ugonjwa mmoja.

Ugonjwa wa Nephrotic syndrome ni hali ya maradhi inayokumba figo na kusababisha kupoteza kiasi kingi cha protini kutoka kwenye damu kuingia kwenye mkojo. Kiasi cha protini kinachopotea ni wastani wa gram 3.5 kwa siku kwa kila mita za mraba 1.73 za mwili.

Chujio za figo (glomeruli) huwa na vitundu vidogo vidogo viitwavyo podocytes ambavyo hufanya kazi ya kuchuja uchafu na sumu nyingine kutoka mwilini na kuzitoa nje. Vitundu hivi vina uwezo wa kuzuia protini isichujwe kuingia kwenye mkojo. Hata hivyo, figo zenye Nephrotic syndrome huwa na podocytes kubwa kiasi cha kuweza kupitisha protini za ukubwa mbalimbali (zikiwepo albumin ambazo ni protini zenye kipenyo kikubwa zaidi). Pamoja na kuharibika huku kwa chujio, podocytes bado hazina ukubwa wa kuweza kupitisha seli nyekundu za damu ndiyo maana mkojo wa mgonjwa wa Nephrotic syndrome hauna damu ndani yake.

Ukubwa wa tatizo

Nephrotic syndrome huathiri karibu watu wa rika zote. Hata hivyo watoto walio katika umri wa miaka 2 mpaka sita ndiyo waathirika wakuu wa ugonjwa huu. Ugonjwa huu umeonekana kuwapata zaidi watoto wa kiume kuliko wa kike.

Visababishi vya Nephrotic syndrome

Visababishi vya Nephrotic syndrome vimegawanyika katika makundi mawili; yale yanayosababishwa na magonjwa yaliyo ndani ya figo zenyewe (primary nephrotic syndrome), au yale yanayosababishwa na magonjwa yaliyo nje ya figo (secondary nephotic syndrome).

Ugonjwa sugu wa figo hutokea pale figo zinazopoteza uwezo wa kutenda kazi unaotokea taratibu na kudumu baada ya kitambo fulani. Hali hii hutokea taratibu, na huchukua muda wa takribani miezi kadhaa hata miaka. Ugonjwa sugu wa figo umegawanywa katika hatua kuu tano, kulingana na ukubwa wa tatizo.

Figo linapopoteza uwezo wake wa kutenda kazi, kusanyiko na limbikizo la maji, uchafu na sumu hutokea mwilini mwa mgonjwa. Aidha kushindwa kufanya kazi kwa figo husababisha pia kutokea kwa maradhi mengine kama vile upungufu wa damu mwilini (anemia), shinikizo la damu (hypertension), ongezeko la tindikali kwenye damu (acidosis), ongezeko la lehemu na mafuta kwenye damu, na magonjwa ya mifupa.

Hatua ya tano ya ugonjwa sugu wa figo hujulikana pia kama kushindwa kufanya kazi sugu kwa figo (chronic kidney disease au end-stage-renal disease).

Tofauti ya Ugonjwa sugu wa figo na kushindwa kufanya kazi kwa figo kwa ghafla (AKI) ni kwamba AKI hutokea ghafla, huchukua muda mfupi kati ya siku hadi wiki kadhaa kuwa tatizo kubwa zaidi. Tofauti nyingine ni kuwa AKI hutokana na tatizo linaloathiri figo moja kwa moja, mishipa yake ya damu au mtiririko wa mkojo unaotoka kwenye figo. Aidha ARF mara nyingi huweza kurekebishwa na mgonjwa akapona kabisa, ingawa kwa baadhi ya wagonjwa sehemu fulani ya figo inaweza isipate nafuu na ikaendelea kudorora kiutendaji kazi.

Hatua za Ugonjwa Sugu wa Figo

Hatua hizi zimegawanywa kulingana na kiwango cha GFR kilichofikiwa na figo husika. GFR kwa kirefu Glomerular Filtration Rate ni kiwango kinachoonesha uwezo wa utendaji kazi wa figo. GFR hupima uwezo wa glomeruli (chujio) la figo katika kuchuja uchafu, maji pamoja na sumu nyingine kwa kila dakika moja kwa mtu mwenye wastani wa urefu wa mita za mraba 1.73. Kadiri jinsi GFR inavyopungua, ndivyo inavyoashiria ukubwa wa tatizo katika figo.

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri

Nje

Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani

Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili. Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?