Kichwa kikubwa ni ugonjwa wa watoto wachanga wa kutanuka chemba za maji za kichwani na hivyo kupeleka muonekano wa kichwa kuwa mkubwa. Ugonjwa huu ni matokeo ya kuzalishwa kwa maji mengi kichwani ama kuziba kwa njia za kupitisha/kufyonzwa maji hayo.
Hutokana na sababu za kinasaba, hivyo mtoto kuzaliwa na kichwa kikubwa. Aina hii huambatana na matatizo mengine kama vile mgongo wazi (SPINE BIFIDA) na mguu kifundo (TALIPES). Sababu nyingine ni maambukizi ya mishipa ya fahamu pindi mtoto anapozaliwa au mara tuu baada ya kuzaliwa.
Ukweli kuhusu kichwa kikubwa
- Asilimia 50 ya watoto wa kichwa kikubwa huwa na changamoto ya ukuaji.
- Kuanza matibabu mapema baada ya mtoto kuzaliwa hupunguza changamoto hizi za ukuaji.
Vihatarishi vyake
- Ukosefu wa virutubisho (vitamins) aina ya folic acid wakati wa ujauzito.
- Unywaji holela wa baadhi ya dawa za hospitali wakati wa ujauzito.
- Ajali, hususani kwa watu wazima
- BAADHI YA WATU WALIOZIDI MIAKA 60 (NORMAL PRESSURE HYDROCEPHALUS)
Dalili zake
Kwa watoto wachanga chini ya umri wa mwaka 1
- Kulialia hovyo
- Kushindwa kunyonya au kula vizuri.
- Kuchelewa kukaza shingo
- Kuvimba/kujaa utosi
Kwa watoto wakubwa na WATU WAZIMA
- Kichwa kuuma
- Kichefuchefu na kutapika
- Matatizo ya kuona, kutembea, balance
- Macho kuzama chini kamaa jua linalokuchwa
Matibabu yake
- Kuwekewa mirija maalum ya kutoa maji (shunt)
- Njia ya kisasa ya matundu (ETV)
Ute wa ukeni ni majimaji yanayotengenezwa na tezi ndogo ndani ya uke na shingo ya kizazi. Majimaji haya huvuja kutoka ukeni kila siku ili kuondoa seli za zamani na uchafu ukeni, kudumisha uke na njia ya uzazi kuwa safi na yenye afya. Ute huu hutofautiana kulingana na rangi, uzito, harufu na hata mtindo wake wa utokaji. Ute huu pia unaweza kuwa na msaada kukuwezesha kujua ishara nyingi ikiwemo siku za uchavushwaji, uwepo wa magonjwa na mengineyo, hivyo katika makala hii itaangalizia aina za ute, ishara gani zinamaanisha kwako kama mwanamke na ni vitu gani vya msingi kuzingatia au ni lini utahitaji msaada wa kitabibu.

Madoa kwenye nguo za ndani?
Kutokwa na ute sehemu za haja ndogo ni jambo la kawaida kabisa kwa wanawake waliopevuka. Ute huu wakati ukiwa unatoka, huwa na rangi nyeupe au mara nyingine usio na rangi kabisa. Lakini, baada ya kukauka mara nyingi huacha madoa (alama)kwenye nguo ya ndani, kama ukiwa umevaa nguo nyeupe utaweza kuona kiurahisi zaidi. Madoa hayo ni kitu cha kawaida kabida kisichohitaji kuwa na hofu ikiwa:
- haina harufu yoyote
- Hauambatani na kuwashwa au uke kuwaka moto
Ikiwa ute unaotoka una harufu mbaya au unahisi kuwashwa au uke kuwaka moto, au una wasiwasi yoyote kuhusu utokaje wake, basi ni muda muafaka kuwasiliana na daktarin wa magonjwa ya wanawake aliye karibu nawe. Pia unaweza kuwashiliana na Daktari wa TanzMED kwa njia ya mitandao.
Muundo wa ute
Kwa maumbile ya mwanamke aliyepevuka, Ute ni majimaji ya kawaida kama vile mate.Lakini kabla hatujaendelea inabidi tujue, kwanini mwili wa mwanamke hutengeneza huu ute? Ute huu ni sehemu ya kawaida katika kulinda na kuhifadhi viungo vya uzazi vya mwanamke.Utando wa ute wa uke na tezi kwenye shingo ya kizazi hutoa majimaji ili kudumisha afya ya viungo vya uzazi.
Kwa kawaida, ute huu huundwa na vitu vifuatavyo, Ute wa njugumono (Mucus secretions) unatengenezwa na tezi za shingo ya kizazi na tezi za Bartholin, Maji maji yanayopita kupitia ukuta wa mishipa (vessel walls) yanayosambaza damu kwenye viungo vya uzazi, Ute unaotengenezwa na tezi za mafuta na tezi za jasho katika sehemu ya nje ya uke, Seluli zilizokufa kutoka kwenye epiteliamu ya uke na shingo ya kizazi, Makoloni makubwa ya bakteria, ikiwa ni pamoja na wale wa manufaa ambao huzuia maambukizi kuzaliana na kudumisha kiwango cha pH cha uke kuwa cha asidi.
Aina za ute
Baada ya kuangalia msingi wa ute na muundo wake, sasa tuangalie aina za ute na maana zake. Ikimbukwe kuwa, kiwango na na aina ya ute unaotoka hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Pia,rangi, muundo, na wingi pia unaweza kubadilika kutoka siku hadi siku, kulingana na hatua ya mzunguko wa hedhi ya mtu:
Siku 1-5: Mwanzoni mwa mzunguko, mara nyingi huwa na ute mwekundu au wa damu wakati mwili unaandaa utando wa damu kwenye mji wa kizazi (uterine lining).
Siku 6-14: Baada ya kipindi cha hedhi, mtu anaweza kugundua ukeni kuna utokaji wa ute kidogo kuliko kawaida. Kadiri yai linavyoanza kuendelea na kukomaa, ute wa shingo ya kizazi utakuwa wa rangi ya mawingu na mweupe . Unaweza kuonekana kuwa wa kunata.
Siku 14-25: Siku chache kabla ya uchavushwaji, ute utakuwa mwepesi na wenye kunata, kama sehemu nyeupe ya yai nyakati hizi kuambatana na ongezeko la hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baada ya uchavushaji, ute utarejea kuwa wa rangi ya mawingu au mweupe ,
Siku 25-28: Ute wa shingo ya kizazi utapungua na mtu atauona kidogo kabla ya kuanza kwa kipindi cha hedhi kingine.
Nyekundu

Hii mara nyingi huwa ni nyekundu iliyopooza au ile inayokaribia rangu ya kutu. Nyekundu mara nyingi ni husababishwa na damu inayotoka wakati wa hedhi. Kwa kawaida, wanawake hupata hadi kila baada ya siku 28, lakini ni jambo la kawaida kupata hedhi kati ya siku 21 hadi 35. Na wengi hukaa kwenye hedhi kwa muda wa siku 3 hadi 5. Endapo utaona damu katika kipindi siyo cha kawaida, basi unashauriwa kuwasiliana na daktari ingawa ni kitendo cha kawaida kwa wanawake wengi kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi (intermenstrual bleeding), kuna baadhi ya muda, inaweza kuwa ni ishara ya tatizo la kiafya.
Kwa mtu yoyote aliyefikia ukomo (monopause) na hajawahi kupata hedhi kwa kipindi cha mwaka mmoja au zaidi, halafu ikatokea akaona ute wa rangi nyekundu / damu ya hedhi, anashauriwa kuonana na daktari haraka kwani inaweza kuwa ni ishara ya ugonjwa wa saratani ya utando wa kizazi (endometrial cancer)
Nyeupe

Ute huu huwa na rangi inayoanzia nyeupe, inaenza maziwa hadi njano. kama hauna dalili nyingine yoyote, basi ute mweupe ni inshara ya ute wa kawaida kama kilainishi shemu ya uzazi. Hata hivyo, ikiwa utoaji wa nyeupe una muundo kama wa jibini , maziwa au unakuja na harufu kali, inaweza kuashiria maambukizi hivyo unatakiwa anapaswa kumwona daktari.
Ute mweupe, mzito, wenye harufu kali mara nyingi unaashiria maambukizo ya fangasi (yeast infection), ambayo pia inaweza kusababisha kuwashwa au kuchomachoma.
Njano-Kijani

Ikiwa ute una rangi ya njano iliyofifia sana, inaweza isiwe ni ishara ya tatizo. Hii inawezekana zaidi, haswa ikiwa rangi hiyo inahusiana na mabadiliko katika lishe au virutubisho vya chakula.
Ikiwa ute una rangi ya njano iliyokoza, au njano-kijani au kijani, inaashiria kuna maambukizi ya bakteria au magonjwa ya zinaa (STI). Tafadhali muone daktari mara moja ikiwa utoaji wa ukeni ni mzito au umegandaganda, au una harufu mbaya.
Pink:

Ute unaweza kuwa pinki iliyopooza au ile iliykoza,. Mara nyingi hii huwa imechanganyika na damu kidogo. Utoaji wa ute wenye rangi ya pinki mara nyingi hutokea kidogo kabla ya kipindi cha hedhi. Lakini, pia inaweza pia kuwa ni kiashiria cha awali cha uwepo wa ujauzito.
Baadhi ya watu wanaweza kutoa damu kidogo baada ya uchavushaji, ambayo pia inaweza kusababisha ute kuwa wa rangi ya pinki. Utoaji wa pinki unaweza kutokea baada ya kufanya tendo la ndoa ikiwa tendo lenyewe limeleta nyufa ndogo au vijijeraha katika uke au shingo ya kizazi.
Hauna Rangi
Ute wa kawaida huwa hauna rangi au mweupeoaji wa kawaida wa ukeni kwa kawaida ni wazi au mweupe. Unaweza kuwa na unyevu au muundo wa utakasa wa yai.
Kijivu

Utoaji wa ute wa rangi ya kijivu sio dalili nzuri kiafya na inaweza kuwa dalili ya maambukizo ya bakteria wanaoitwa bacterial vaginosis (BV).
Kawaida, maambukizi ya bakteria wa BV huambatana na dalili nyingine, ikiwa ni pamoja na:
- Kuwashwa
- Kuhisi kuchomwachomwa
- Harufu kali
- Kuvimba karibu na vulva au sehemu ya nje ya uke
Mtu yeyote mwenye ute wa kijivu anapaswa kumwona daktari mara moja. Baada ya kuthibitisha ugonjwa huo, kwa kawaida daktari humpa mgonjwa dawa za kuua bakteria (antibiotiki) kwa ajili ya matibabu ya BV. Epuka kutumia madawa ya antibiotiki bila kuandikiwa na daktari kwani kila dawa hutumia kulingana na ukubwa wa tatizo, aina ya ugonjwa na sababu nyingine zaidi za kitabibu ambazo huamuliwa na daktari baada ya kuona hali halisi ya ugonjwa na mgonjwa.
Mwanamke anaweza kuona ute msafi, unaoteleza sana siku chache kabla ya cuhavushaji (ovulation), wakati wa kujamiiana, na wakati wa ujauzito.
Je ni kwa kiwango gani huwa ni kawaida?
Kwa mwanamke mwenye Afya njema, kwa kawaida hutoa wastani kati ya mililita 1 hadi 4 ya ute kila ndani ya masaa 24. Hata hivyo, kiasi hicho kinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu, kwa hvyo ikiwa utapata zaidi ya hapo inawezekana kabisa ni kawaida.
Pia, ni muhimu kukumbuka kwamba utoaji wa ute huongezeka sana wakati wa uchavushaji (kuwa na ute mwingi), ujauzito, na unapotumia vidonge vya uzazi wa mpango.
Ute wakati wa kujamiiana
Lengo kuu la ute kwenye sehemu za siri za mwanamke ni kufanya kuwe na unyevunyevu. Lakini ute huu wa kawaida hata pale unapokuwa umetoka katika kiwango chake cha juu kabisa (sanasana wakati wa uchavushaji), bado hauna uwezo wa kufanya sehemu za siri kuwa zimeloa vya kutosha kwa ajili ya kitendo cha kujamiiana. Hivyo kunahitajika ute mwingine wa ziada kuhakikisha kunakuwa na mtelezo wa kutosha.
Wakati wa tendo la ndoa, sehemu kubwa ya kiungo cha uzazi cha mwanamke kinakuwa kimepata damu ya kutosha hivyo hufanya vijimishipa vya shemu hii kutanuka kitendo kinachosababisha majimaji kupita kwa urahisi. Tezi za Bartholin zinazopatikana kwenye mashavu ya uke (ulvar vestibule) pia tezi za Skene zinazopatikana kwenye mrija wa mkojo (urethra) zote zinatumika kutengeneza ute ute.
Uteute huu husaidia kuongeza mtelezo wakati wa tendo la kujamiiana na kupunguza michubuko na msuguano wakati wa tendo.Kiwango halisi cha ute ute huu hutegemeana na mtu, umri, kiwango cha homoni and tarehe za hedhi.
Wakati gani nimuone daktarin?
Unatakiwa kuwahi kumuona daktari ikiwa utahisi ute una harufu au muonekano ambao sio wa kawaida.Pia anapaswa kutafuta huduma ya matibabu ikiwa unapata dalili kama vile:
- Kuwashwa
- Maumivu au kujisikia vibaya
- Ute unaofanana na jibini cha krimu
- Kutokwa damu kati ya hedhi au baada ya ukomo wa hedhi
- Kutoka damu mara kwa mara baada ya tendo la ndoa
- Ute wa rangi ya kijivu, kijani, au manjano
- Harufu kali ukeni
- Maumivi makali wakati wa kukojoa
Daktari atafanya uchunguzi wa viungo vya uzazi vya mwanamke (pelvic exam). Wanaweza pia kuhitaji kuchukua sampuli ya ukeni kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara.
Maswali ya Mara Kwa Mara: (FAQ)

Je, ni kawaida kwa wasichana wadogo kutokwa na ute?
Ndiyo, wasichana wa kila umri wanaweza kutokwa na ute, kawaida kwa kiasi kidogo hadi wanapokaribia kuingia kwenye umri wa kupevuka (Kuvunja ungo). Pia, huwa unatofautiana katika kiasi na rangi (kutoka hamna rangi hadi manjano au nyeupe). Hakuna haja ya wasiwasi isipokuwa ikiwa haueleweki, una rangi nyingine, au harufu isiyo ya kawaida.
Nawezaje kuzuia ute?
Utoaji wa ute ni jambo la kawaida na muhimu kwa afya ya uzazi wa kike. Hakikisha hamna harufu, au rangi zisizo za kawaida, pia ukiwa hauwashwi hauoni au kuchomwachomwa, hakuna haja ya kuchukua hatua yoyote.
Je, utokaji wa ute ni dalili ya ujauzito?
Ikiwa utokaji wa ute umeongezeka kwa kiasi na ni mwepesi, wa maziwa, na una harufu nyepesi, inaweza kuwa dalili ya ujauzito wa awali. Hii inaitwa leukorrhea na inaweza kujitokeza mapema kama wiki moja hadi mbili baada ya kushika ujauzito. Wakati wa ujauzito, utoaji wa ute utabadilika kulingana na muundo, kujirudia (frequency), na kiasi.
Umri gani Wasichana wanaanza kutokwa na ute?
Kwa kawaida wasichana huanza kupevuka kuanzia miaka 8 hadi 13. Lakini, baadhi ya vijana huanza kuonyesha dalili za ujana nje ya muda huo. Kwa ujumla, hedhi huanza takriban mwaka mmoja baada ya kuvunja ungo, ambayo mara nyingi hutokea akiwa bado mdogo sana.
Ni rangi gani ya ute inayohusiana na fibroids?
Fibroid ya kizazi (pia inaitwa leiomyoma, fibromyoma, au myoma) kwa kawaida ni ukuaji usio wa kansa ndani ya kizazi. Ute unaohusiana na fibroids unaweza kuwa kuanzia usio na rangi hadi mweupe au rangi ya damu hadi kijivu au kahawia. Kutokwa na damu nje ya kipindi cha hedhi ni jambo la kawaida kwa watu wenye fibroids.
Nini husababisha utokaji wa ute mwingi?
Utoaji wa ute zaidi ya kiwango cha kawaida inaweza kuwa ishara ya:
- uchavushaji
- Athari ya mzio
- Msongo wa mawazo
- Homoni kutokuwa kwa uwiano
- Matumizi ya antibiotics
- Matumizi ya dawa za kuzuia mimba
Je, ute mweupe ni ishara ya hedhi?
Ndiyo, ute mzito, mweupe, wa maziwa ni ishara ya kawaida ya kukaribia kipindi cha hedhi kinakaribia. Hiyo ni matokeo ya viwango vya juu vya progesterone, homoni inayosimamia ujauzito na mzunguko wa hedhi. Aina hii ya utokaji wa ute inaaminika kuwa ni ya kawaida ikiwa haiendani na harufu mbaya. Kwa kulinganisha, wakati viwango vya estrogeni vinaongezeka, ute huwa huwa hauna rangi na unavutika.
Kwa kawaida, meno ya mtoto ya utotoni (meno ya awali) huanza kutoka kuanzia miaka 6. Kwa baadhi ya watoto, huweza kuchelewa kuanza kutoka meno ya utotoni hadi wanapoanza mwaka wA 7.
Meno ya kwanza yanayoanza kutoka ni yale mawili ya chini ya kati (lower central incisors) na hufuatiwa na yale ya juu ya kati (upper central incisors) (. Baada ya hapo, hufuatiwa na meno ya kutafunia ya kwanza na ya pili.

Kwa kawaida, meno ya ya awali hukaa bila kutoka mpaka pale meno ya kudumu yanapotaka kuanza kuchomoza, hivyo hulisukuma jino la utoto na kusababisha kutoka. Endapo mtoto atatoka meno mapema au jino litatoka kwa sababu ya ajali au kuoza, basi jino la kudumu litaziba pengo hilo baada ya muda kufika. Hii inaweza kusababisha meno kutokuwa na mpangilio mzuri kwakuwa wakati linachomoza kulikuwa na meno mengine ya utotoni, hivyo unashauri kuwasiliana na daktari wa kinywa na meno kwa ushauri zaidi.
Pale mtoto anapoanza kutoka meno, tafadhali zingatia kanuni bora za Afya ya kinywa na meno kama ;
- Kuhakikisha anasubua meno angalau mara mbili kwa siku. Mkazanie kwa sababu umakini unahitajika.
- Msaidie mtoto kusugua meno kila siku
- Hakikisha anakula chakula bora na kupunguza matumizi ya vyakula vitamu
- Weka miadi na daktari wa kinywa nameno
Kwa mazingatio haya, utaweza kuhakikisha afya bora ya kinywa na meno ya mtoto wako. Pia, unaweza kusoma makala zaidi juu ya Afya ya kinywa na meno wakati wa makuzi ya mtoto
Afya bora ya kinywa na meno kwa mtoto ni muhimu sana na ina uhususiano wa moja kwa moja na afya yake kwa ujumla. Humuepusha mtoto kupata maumivu, uwezekano wa uambukizo, kumfanya aweze kutafuna vizuri ili kupata virutubisho muhimu kwa ajili ya kujenga kinga dhidi ya magonjwa, na kusaidia ukuaji. Afya nzuri ya kinywa na meno pia itamfanya mtoto aweze kuhudhuria masomo ipasavyo na hivyo kupata matokeo mazuri.
Umuhimu wa meno ya utoto
Wazazi /walezi wengi hujiuliza kwanini wahangaike kutunza meno ya utoto ambayo yanatarajiwa kung’oka na kuota ya ukubwa. Meno ya utoto ni muhimu kutokana na sababu zifuatazo:
Humsadia mtoto kutafuna na hivyo kumwezesha kupata virutubisho muhimu
Hutunza nafasi kwa ajili ya meno ya ukubwa
Hali ya afya ya meno ya utoto huathiri hali ya afya ya meno ya ukubwani
Husadia uumbaji wa maneno (kuongea)
Kama mzazi / mlezi unatakiwa kuwa mstari wa mbele kutunza meno ya mtoto wako kwani, watoto hupenda kujifunza kutokana na mfano wa wazazi.
Zifuatazo ni dondoo muhimu kwa wazazi/walezi kwa ajili ya kutunza afya bora ya mtoto:
Umri wa kuzaliwa mpaka miezi 6
- Mnyonyeshe mtoto maziwa ya mama pekee hadi umri wa miezi sita.
- Maziwa ya mama ni muhimu sana kwa ukuaji na kinga dhidi ya magonjwa.
Umri wa miezi 7 hadi miezi 18
- Usimlaze mtoto akiwa na chuchu ya maziwa au chuchu ya mama mdomoni ili kuzuia ugonjwa wa kuoza kwa meno (rampant caries)
- Mpatie mtoto maji badala ya juisi akiwa na kiu.
- Iwapo utampa mtoto juisi ya boksi unashauriwa kuongeza kiwango cha maji sawa na kile cha juisi ili kupunguza kiasi cha sukari kilichomo ndani ya juisi.
- Ukitengeneza juisi nyumbani kwa ajili ya mtoto, jiepushe kuiongezea sukari.
- Jino la kwanza litakapoota, anza kusafisha kinywa cha mtoto kutumia kitambaa laini kilicholoweshwa kwenye maji safi au mswaki laini bila dawa.
- Panga miadi ya kwanza ya kumwona daktari wa meno (first appointment) wakati mwanao hana maumivu au shida yoyote ili kujenga mahusiano mazuri kati ya mtoto na daktari
Umri wa miezi 18 hadi miaka 6
- Dhibiti ulaji wa vyakula vyenye sukari na zingatia ulaji wa vyakula vinavyojenga afya ya mtoto kama matunda, mboga mboga, karanga, maziwa na samaki.
- Safisha meno ya mtoto kutumia maji safi na mswaki laini na dawa ya meno (zingatia kiwango cha dawa: kiasi cha mbegu ya kunde) asubuhi na jioni kila siku.
- Mtoto asukutue mdomoni ili kupunguza kiwango cha dawa itakayobaki.
- Chunguza mara kwa mara meno ya mtoto ili kugundua dalili za mwanzo za ugonjwa wa kuoza kwa meno (rangi kuwa nyeupe au kahawia zaidi katika eneo husika baada ya kukausha) na pia matatizo mengine kama uvimbe, vijipu au kutoka damu kwenye fizi.
- Mpeleke mtoto kwa daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka na mara unapogundua tatizo lolote kinywani mwake.
Umri wa miaka 6 hadi 12
- Msimamie mtoto kusafisha kinywa na meno mara mbili kwa siku.
- Mtoto ateme dawa itakayobaki ila asisukutue na maji baada ya kupiga mswaki.
- Mjengee mtoto tabia ya kusukutua na maji kila baada ya kula vyakula vyenye sukari kama keki, chokoleti au juisi.
- Chunguza mara kwa mara meno ya mtoto ili kugundua dalili za mwanzo za ugonjwa wa kuoza kwa meno na matatizo mengine kinywani.
- Mpeleke mtoto kwa daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka na mara unapogundua tatizo lolote kinywani mwake.
Umri wa miaka 12 na zaidi
- Mtoto anaweza kuanza kusafisha kinywa na meno bila ya usimamizi.
- Dhibiti ulaji wa vyakula vyenye sukari na zingatia ulaji wa vyakula vinavyojenga afya ya mtoto kama matunda, mboga mboga, karanga, maziwa na samaki.
- Mpeleke mtoto kwa daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka na mara unapogundua tatizo lolote kinywani mwake.
CREDIT: Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS)
Kumekuwa na taarifa mbalimbali zinazoripotiwa hapa nchini kuhusu watoto wanaozaliwa wakiwa wameungana. Jamii ya watanzania itawakumbuka sana watoto wa aina hiyo waliofahamika kwa majina ya Mariamu na Consolata ambao kwa sasa ni marehemu.Watoto hawa walikuwa faraja kubwa kwa taifa baada ya kuweza kuishi na kusoma hadi ngazi ya kuingia Chuo Kikuu.
Aidha kumekuwa na riporti za watoto wengine walioungana hapa nchini. Ripoti hii ilitolewa na zahanati ya St. Theresa Health Centre iliopo Kyaka wiliyani Misenye.
Tafiti zinaonyesha kwenye kila uzao wa 50,000-200,000 kunakuwepo na pacha moja iliyoungana. Mara nyingi huzaliwa wamekufa na wengine hufa kipindi kidogo tu baada ya kuzaliwa na wengine huweza kuishi kwa kipindi fulani. Aina hii ya pacha hutokea zaidi kwa jinsia ya kike kwa uwiano wa 3:1 na jinsia ya kiume.
Tafadhali tuungane pamoja katika makala hii ili tujifunze kuhusu watoto hawa wanaozaliwa huku wameungana.
Watoto walioungana (conjoined twins) ni mapacha ambao maumbile yao yameungana tangu wakiwa katika mfuko wa uzazi na baada ya kuzaliwa. Hali hii hutokea kufuatia kuungana au kutokugawanyika kwa yai lililopevushwa wakati wa ukuaji wa awali.
Kawaida yai moja lililopevushwa hugawanyika zaidi katika siku ya 13 baada ya yai hilo kupevushwa (monozygotic twin pregnancy).Kutokugawanyika kwa yai hili lililopevushwa husababisha mapacha kuzaliwa wakiwa wameungana.Kuna aina mbili za mapacha walioungana;
- Mapacha wanaotumia kondo moja la nyuma (single placenta) hujulikana kama monochromic twins au
- Mapacha wanaotumia amniotic sac moja hujulikana kama monoamniotic twins
Mapacha walioungana husababishwa na kushindwa kuungana au kutengana kwa yai liliopevushwa wakatii wa ukuaji wa awali, japo hii haiwezi kuelezea kila aina ya kuungana (conjuction)
Ziko aina nyingi za mapacha walioungana (conjoined twins) na wanaweza kuwekwa kwenye makundi makubwa mawili;
- Non dorsally conjoined twins- Aina hii ya mapacha walioungana huchangia kitovu kimoja (umbilical cord) moja na baadhi ya viungo vya ndani ya mwili (internal organs)
- Dorsally conjoined twins -Hapa kila pacha anakuwa na (umbilical cord ) yake na mara nyingi hawachangii viungo vya ndani ya mwili.Hii hutokea pindi pacha hawa wamegawanyika na baadaye kuugana tena ( secondary fusion) katika hatua ya ukuaji wa awali.
Pathofiziolojia
Pacha hawa hutokea baada ya mgawanyiko (cleavage or axis duplication) kutokea baada ya siku ya 13 ya kupevushwa kwa yai. Inaaminika kawaida mgawanyiko huu hutokea siku ya 8 hadi ya 12. Sasa ukitokea baada ya hapo mgawanyiko huo ukianza huishia njiani hivyo husababisha aina hii ya mapacha.
Tafiti nyingine husema pacha waliogawanyika vizuri wanaweza kuungana tena katika hatua za awali za ukuaji kwenye mfuko wa uzazi na kupelekea aina hii ya pacha.
Kisababishi cha matukio haya kutokea bado hakijulikani.
Zifuatazo ni aina za mapacha walioungana (conjoined twins)
Thoraco-omphalopagus-Aina hii ya pacha wameungana kifuani na kwenye tumbo. Hii ndo aina inayoonekana sana kwa asilimia 28. Mara nyingi hawa huchangia moyo mmoja, ini (liver) na hata sehemu ya juu ya utumbo (upper intestine).
Thoracopagus- Aina hii ya pacha wameungana kifuani tu. Ndo aina inafuatia na hutokea kwa asilimia 18. Wanaweza kuchangia moyo mmoja na ini.
Omphalopagus- Aina hii ya pacha huungana tumboni karibu na kitovu. Aina hii hutokea kwa asilimia 10. Hawa huchangia ini moja na sehemu ya utumbo mkubwa (colon) na utumbo mdogo wa chini.
Heteropagus (Parasitic twins). Aina hii nayo hutokea kwa asilimia 10. Aina hii kunakuwa na pacha mmoja mwenye hitilafu ameungana na pacha mwingine mzima.
Craniopagus- Aina hii hutokea kwa asilimia 6. Vichwa vinakuwa vimeungana. Na mara nyingi wachangia ubongo mmoja.
Ziko aina nyingine ambazo hutokea mara chache sana kama zifuatavyo;
Pyopagus- Aina hii mapacha wanaungana kwenye mgogo wa chini na makalio. Hawa huweza kuwa wanachangia sehemu ya utumbo na sehemu za siri mfano uume au uke
Rachipagus -Aina hii mapacha wameungana nyuma kwenye mgongo wote juu hadi chini.
Ischiopagus- Aina hii ya mapacha wameungana kwenye nyonga upande au uso kwa uso. Pacha hawa wanaweza kuchangia utumbo wa chini na sehemu za siri. Pia wanaweza changia miguu miwili au mitatu.
Cephalopagus- Aina hii ya mapacha wanaungana kuanzia kwenye kichwa hadi kwenye kitovu. Aina hii hi ngumu kuishi.
Historia ya mama
Mama wa mapacha aina huu hana tofauti na mama mwenye mapacha wa kawaida. Hamna dalili yoyote ya tofauti kwake.
Uchunguzi
Mapacha hawa wanaweza kugundulika kwa kipimo cha ultrasound mwanzo kabisa mwa ujauzito. Au kwa kutumia Prenatal Magnetic Resonance imaging (MRI)
Tiba
Mapacha wanaoishi baada ya kujifungua wanaweza wekwa kwenye makundi makuu mawili
- Wale ambao wanaweza kutenganishwa kwa upasuaji
- Wale wasioweza kutenganishwa kwa upasuaji
Kwenye tiba ya upasuaji uchunguzi wa kina unafanywa ili kubaini uwezekano wa kuwatenganisha hasa kama wanachangia baadhi ya viungo muhimu kama moyo. Upasuaji wa kuwatenganisha mapacha walioungana uhusisha timu za wataalamu wa afya wabobezi kutoka fani mbalimbali za afya. Wakati mwingine upasuaji unaweza sabibisha pacha mmoja ua wote kupoteza maisha.
Tanzania ilishafanikiwa kufanya upasuaji wa aina hii wa kutenganisha mapacha walioungana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili National Hospital(MNH)
Picha: BBC
Je unafahamu inakadiriwa kuwa, mwanamke hupata hedhi wastani wa mara 400 katika maisha yake? Pia, neno linalotumika sana kuwakilisha hedhi ni "period", neno hili lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye miaka ya 1822 likimaanisha tukio linalotokea ndani ya muda fulani au linalojirudia baada ya muda fulani. Leo hii tuangalie mambo mengine 5 muhimu kuyajua kuhusiana na hedhi.
1. Kwa wastani, mwanamke huanza kupata hedhi yake ya kwanza kabisa akiwa na umri wa miaka 12.
2. Mzunguko wa siku za hedhi huwa kati ya siku 21 hadi 35. Ingawa wengi huwa na mzunguko wa siku 28, lakini kuzidi wiki moja au kuwahi kwa wiki moja ni kitu cha kawaida.
3. Mwanamke huzaliwa na mayai milioni 1 hadi 2. Mayai haya, mengi hufa jinsi mwanamke anavyoendelea kuishi na ni mayai 400 tu ndiyo hukadiriwa kufika hatua ya ukomavu tayari kwa uchavushwaji.
4. Msichana anaweza kupata ujauzito kabla ya kuanza hedhi yake ya kwanza. Hii ni kwa sababu, yai huanza kukomaa kabla ya kuona hedhi yake ya kwanza, hivyo kama atashiriki tendo bila kinga, kuna uwezekano wa kupata ujauzito.
5. Wanawake wengi hufikia ukomo wa kupoata hedhi (menopause) wakiwa na umri wa miaka 48 hadi 55.
Utafiti uliofanyika nchini Uingereza kwa kuhusisha wanawake 46,000 umesema ya kwamba matumizi ya dawa za uzazi wa mpango hupunguza hatari ya kupata saratani ya mayai ya mwanamke (ovarian cancer), saratani ya mfuko wa kizazi (uterine cancer) na ya utumbo mpana wa chakula (bowel cancer).Watafiti hao wamesema kinga anayopata mwanamke dhidi ya saratani hizi kutokana na matumizi ya dawa hizi za uzazi wa mpango ni ya muda mrefu mpaka miaka 35 baada ya mwanamke huyo kuacha kutumia dawa hizi za uzazi wa mpango.
Katika utafiti huu, wanawake wa Uingereza walitumia dawa hizi za uzazi wa mpango kwa wastani wa miaka mitatu na nusu wakati wakiwa na umri kati ya miaka 20 mpaka miaka 30.Kinga dhidi ya saratani kwa wanawake hawa waliotumia dawa hizi za uzazi wa mpango kipindi cha ujana wao ilionekana kuwepo mpaka walipotimiza miaka 50, 60 na 70, umri ambao wanawake wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata saratani.
Watafiti hawa kutoka chuo kikuu cha Aberdeen nchini Uingereza,waliendelea kusema ya kwamba wanawake waliotumia dawa za uzazi wa mpango walikuwa na hatari pungufu ya theluthi moja kupata saratani ya mayai ya mwanamke au saratani ya ukuta wa mfuko wa kizazi cha mwanamke (endometrial cancer).Pia wanawake hawa waligundulika kuwa na hatari pungufu ya moja ya tano kupata saratani zozote zile ikilinganishwa na wanawake ambao hawakutumia dawa hizi za uzazi wa mpango.
Karibia wanawake milioni 3.5 nchini Uingereza hutumia njia hii ya uzazi wa mpango kama njia rahisi kwao. Utafiti huu uliochapishwa katika jarida la American Journal of Obstetrics and Gynaecology utabadilisha mtazamo wa watu kuhusu athari na faida za dawa hizi za uzazi wa mpango.
Mara nyingi wanawake wameambiwa ya kwamba dawa za uzazi wa mpango zinawaweka kwenye hatari ya kupata saratani ya matiti au ya shingo ya kizazi (cervical cancer) lakini utafiti huu umeonyesha hatari hii huondoka kabisa ndani ya miaka mitano baada ya mwanamke kuacha kutumia dawa hizi za uzazi wa mpango.Wakati mwanamke anapotimiza umri wa kukoma kupata hedhi, kipindi ambacho kwa kawaida huongeza hatari ya kupata saratani za aina tofauti tofauti, lakini kwa wale ambao walitumia dawa za uzazi wa mpango hapo awali hawako kwenye hatari yoyote ile ya ziada ya kupata saratani, walisema watafiti hao kutoka nchini Uingereza.
Fibroids ni moja ya matatizo yanayowasumbua wanawake wengi , kwa lugha ya kawaida, Fibroids maana yake ni uvimbe wa msuli wa kifuko cha uzazi. Uvimbe huu unaweza kuwa na ukubwa tofauti kuanzia kama punje ya harage mpaka ukubwa wa nazi. Wakati mwingine unaweza kudhani ni ujauzito!
Sio kila mwenye fibroids anakuwa na matatizo kiafya. Zinaweza kuwepo miaka mingi bila matatizo yoyote. Hata hivyo inashauriwa kila mwenye fibroids awe anapimwa na daktari angalau mara moja kwa mwaka ili kuona jinsi zinavyoendelea na kuhakikisha kuwa hazikui kwa kasi au kuhatarisha kuwa kansa.
Kwa wale zinaowaletea matatizo, fibroids husababisha kutokwa na damu nyingi za hedhi, maumivu ya tumbo, mimba kuharibika zikiwa changa, kuzaa watoto njiti na fibroid kukandamiza viungo vingine kama kibofu cha mkojo na kusababisha kukojoa mara kwa mara au matatizo ya haja kubwa.
Njia ya kugundua uwepo wa fibroid ni kupimwa na daktari na kufanyiwa ultrasound.
Matibabu yake yapo ya aina kuu tatu:
1. Kunywa dawa. Hata hivyo dawa zilizopo sasa hazina matokeo mazuri kuondoa fibroids ila husaidia kupunguza ukuaji wake.
2. Kuiondoa fibroid kwa operation. Ziko aina nyingi za operation kupitia kwenye tumbo au kupitia ndani ya kifuko cha uzazi. Aina ya operation hutegemea mahali ilipo fibroid.
3. Kuondoa kifuko cha uzazi. Njia hii huwafaa wale ambao hawana mpango wa kupata mtoto.
Kuna nadharia mbalimbali juu ya vitu vinavyosababisha fibroids lakini hakuna kitu kilichothibitika moja kwa moja kuwa chanzo cha fibroids. Kwa wale wenye uzito mkubwa inashauriwa kupunguza mwili kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata fibroids.
Zipo tafiti zinazoonyesha kuwa matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango vinapunguza uwezekano wa kupata fibroids.
Kunyonyesha kuna faida nyingi sana kwa mtoto mchanga pia na kwa mama. Na mara nyingi hili huwa ni umamuzi wa mtu binafsi ila ushauri wa msisitizo unatolewa na chama cha madaktari wa watoto na chama cha madaktari wa magonjwa ya wakina mama vyote vya marekani.
Faida kwa Mtoto
- Virutubisho vilivyomo kwenye maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga , maana maziwa ya mama huwa uwiano mzuri wa vitamin, protini, na mafuta mazuri na kumuwezesha mtoto kukuwa vizuri
- Vilevile maziwa ya mama huwa na virutubisho vyenye uwezo wa kumkinga mtoto kupata magonjwa kitaalamu antibodies, ambavyo humkinga mtoto mchanga dhidi ya vimelea (bakteria na virusi)
- Maziwa ya mama hupunguza uwezekano wa mtoto mchanga kupata pumu au aleji
- Na vilevile watoto wakinyonyeshwa kwa miezi sita mfululizo bila kuchanganyiwa na vyakula vingine hupunguza hatari ya kupata maambukizi ya masikio, mfumo wa hewa na magonjwa ya kuharisha
- Kuna tafiti ambazo zinaonyesha maziwa ya mama yanaongeza upeo wa kufikiri wa mtoto atakapo kua
Watoto ambao hula chakula cha usiku pamoja na familia yao wanakuwa na afya njema kiakili na kimwili na wana uwezekano mdogo wa kupenda kunywa soda na vyakula hatarishi kwa afya (fast food)
Watafiti kutoka nchini Canada wanasema, watoto ambao mara kwa mara hula chakula pamoja na familia zao wanakuwa na afya njema ya kiakili na kimwili ukilinganisha na watoto ambao hawapati nafasi ya kula chakula pamoja na familia zao.
Watafiti hao wamegundua ya kwamba watoto hao wanapofikisha umri wa miaka 10 wanakuwa na afya njema kiakili, wachangamfu na uwezekano mdogo sana wakunywa vinywaji vyenye sukari kama soda ikiwa watakula chakula mara kwa mara pamoja na wazazi, ndugu au walezi wao.
Utafiti huu ulifanyika kwa muda wa miaka 10, na ulihusisha kuwafuatilia watoto tokea wakiwa wachanga mpaka walipotimiza umri wa miaka 10.
Watafiti hao wanasema,matokeo yao yanathibitisha ile dhana ya kwamba,kula chakula kwa pamoja kama familia ni muhimu sana kwa binadamu na huleta manufaa mbalimbali kwa sababu hujumuisha vipengele vyote muhimu sana vya mfumo wetu maisha pamoja na afya za wazazi wetu.
Uwepo wa wazazi wakati wa kula chakula huwapatia nafasi muhimu sana watoto ya kujifunza kujumuika na wengine, kujadiliana kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii na kutoa duku duku zao za kila siku na ni fursa adhimu ya kujifunza mijumuiko ya kifamilia kwenye mazingira wanayoyafahamu na salama kiakili’’ alisema Professor Linda Pagani, mtaalamu wa wa elimu ya kiakili kutoka Chuo Kikuu cha Montreal, Canada.

