Image

Tezi Dume (Prostate gland)

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.

Kuvimba Tezi Dume (BPH)

Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.

Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.

Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.

KWA kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo zimehifadhiwa katika mfuko maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo cha maji kinachozunguka korodani ili kuilinda. Mwanaume endapo atakuwa na korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo kubwa.

Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume anaweza kuwa na korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana na matatizo mbalimbali.

Mwanaume mwenye korodani moja anaweza kuzalisha mbegu au asizalishe kabisa, kitu cha msingi akapimwe hospitali kuona uwezo wa hiyo moja. Mwanaume ambaye hana korodani kabisa hawezi kuzalisha mbegu za uzazi hivyo hana uwezo wa kumpa mimba mwanamke. Tatizo la kuwa na korodani moja au kukosa kabisa tutakuja kuliona katika makala zijazo.

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA

Maumivu ya korodani hutokea katika korodani au haswa moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi. Maambukizi haya yanaweza kuwa makali na ya muda mfupi,yanakuwa makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena yakiwa makali sana kama mwanzo au pia huwa sugu yaani unakuwa na maumivu ambayo siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayokunyima raha.

Maumivu ya korodani yanaweza kuwa makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa ‘Fournier's gangrene' au inatamkwa ‘Fonias gangrini'.

Vilevile inaweza kutokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha ukapata maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni, tatizo hili linaitwa Testicular Torsion. Matatizo haya kwa ujumla wake tutakuja kuyaona katika makala zijazo.

CHANZO CHA TATIZO

Maumivu ya korodani yana vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua takriban zaidi ya miezi mitatu. Maumivu makali na ya ghafla huwa hayavumiliki na huwa na tiba ya dharura. Maumivu haya sugu huwa kwa kipindi fulani hasa kwa wanaume ambao wametoka kufunga uzazi Vesectomy lakini baadaye hupoa. Vilevile husababishwa na maambukizi katika korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits, Prostatis na Orchitis ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume na husababisha ugumba.

PUMBU.jpg

 

Maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria (Chronic non-bacterial prostatitis)

Kama jina lake linavyoeleza, maambukizi ya aina hii kwenye tezi dume husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo katika vichocheo vya mwili (homoni) na hata matatizo katika mfumo mzima wa neva.Pia kumekuwepo na dhana ya kwamba maambukizi ya aina hii huchangiwa  na kuwepo kwa maumivu ya kibofu cha mkojo yanayotokana na maambukizi katika kibofu hicho (Cystitis) au hali ya hewa hususan baridi ambayo huongeza maumivu ya tezi dume na hali ya joto ambayo hupunguza maumivu hayo. Baridi pia huchangia kujirudia kwa dalili na viashria vya maambukizi haya. Katika utafiti uliofanyika kaskazini mwa nchi ya Finland (nchi ambayo ina majira ya baridi kali sana),umeonyesha ya kuwepo kwa maambukizi ya aina hii yanayoambatana na dalili na viashiria vyake kali sana kuliko sehemu yoyote duniani.

Maambukizi haya ya tezi dume bila uwepo wa bakteria hutokea kwa wanaume walio katika umri wa miaka 35-45 na inakisiwa kutokea kwa asilimia 90-95 ya maambukizi yote ya tezi dume .

Prostatitis ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi  ya vimelea vya bakteria katika tezi dume (prostate) kwa wanaume.

Kuna aina kuu nne za ugonjwa huu wa prostatitis

1. Maambukizi ya ghafla ya tezi dume (Acute bacterial prostatitis)

2. Maambukizi sugu ya tezi dume (Chronic bacterial prostatitis)

3. Chronic prostatitis without infection/Chronic pelvic pain syndrome/chronic non bacterial prostatitis

4. Asymptomatic inflammatory prostatitis 

Tuangalie aina moja baada ya nyingine za ugonjwa huu 

Maambukizi ya ghafla ya tezi dume (Acute bacterial prostatitis)

Ni maambukizi ya tezi dume yanayosababishwa na vimelea vya bakteria aina ya E.coli, Klebsiella, Proteus, Pseudomonas, Enterobacter, Staphylococcus aureus, Enterococcus, Serratia na vimelea vinavyosababisha magonjwa ya zinaa. Maambukizi haya yanaweza kufika katika tezi dume moja kwa moja kupitia kwenye damu, au kutoka kwenye kiungo kilicho na maambukizi karibu na tezi dume au huweza kufika kwenye tezi dume kutokana na athari za kufanyiwa kipimo cha kuchukua nyama ya tezi dume kuipeleka  maabara kwa uangalizi zaidi au kwa lugha ya kitaalamu tunaita prostate biopsy. 

Dalili na viashiria vya maambukizi ya ghafla ya tezi dume

     - Homa

     - Kuhisi baridi

     - Kutetemeka kutokana na baridi

     - Maumivu chini ya mgongo 

     - Maumivu katika maeneo ya sehemu za siri

     - Kupata haja ndogo /kukojoa mara kwa mara

     - Kupata haja ndogo wakati wa usiku inayomfanya mtu kushindwa kuivumilia na hivyo kukimbia chooni

     - Maumivu/kichomi wakati wa kukojoa/haja ndogo

     - Maumivu ya mwili mzima